الطلاق
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَسْكِنُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ سَكَنتُم مِّن وُجْدِكُمْ وَلَا تُضَآرُّوهُنَّ لِتُضَيِّقُوا۟ عَلَيْهِنَّ ۚ وَإِن كُنَّ أُو۟لَـٰتِ حَمْلٍ فَأَنفِقُوا۟ عَلَيْهِنَّ حَتَّىٰ يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ فَإِنْ أَرْضَعْنَ لَكُمْ فَـَٔاتُوهُنَّ أُجُورَهُنَّ ۖ وَأْتَمِرُوا۟ بَيْنَكُم بِمَعْرُوفٍ ۖ وَإِن تَعَاسَرْتُمْ فَسَتُرْضِعُ لَهُۥٓ أُخْرَىٰ ٦
{6} Imetajwa hapo awali kuwa Mwenyezi Mungu amekataza kuwatoa wanawake waliopewa talaka majumbani, na hapa akaamrisha wawekwe nyumbani kwa wema. Nayo ni nyumba ambayo watu kama yeye na kama mkewe huishi. Kwa mujibu wa kiasi awezavyo mume. "Wala msiwaletee madhara kwa kuwapa dhiki" kwa kauli au vitendo. Ili wapate kuchoka na kuondoka nyumbani kabla ya kumaliza eda yao, na hapo mnakuwa ndio mumewatoa. Jumla ya hayo ni kwamba aliwakataza kuwatoa na akawakataza kutoka nje, na akawaamrisha kuwafanya waishi katika njia ambayo haitawaletea madhara wala taabu, na hilo ni kulingana na desturi. "Na wakiwa wana mimba, wagharimieni mpaka wajifungue." Hilo ni kwa sababu ya mimba iliyomo tumboni mwake ikiwa ni mwanamke aliyetalikiwa talaka isiyo ya kurudiana, na kwa sababu yake mwenyewe na mimba yake ikiwa ni talaka ya kurudiana, na mwisho waa matunzo hayo ni mpaka ajifungue. Basi wakishajifungua, ima watawanyonyesha watoto wao au la. "Na wakikunyonyesheeni, basi wapeni ujira wao" kama walivyosikilizana ikiwa watasikilizana juu ya kiwango maalumu. Vinginevyo, basi atapewa ujira kama ule wanaopewa mfano wake. "Na shaurianeni kwa wema" wenye manufaa na masilahi katika dunia na akhera. Kwa maana kughafilika katika kushauriana yaliyo mema kunasababisha madhara na maovu anayojua Mwenyezi Mungu pekee. Na katika kushauriana kuna ushirikiano katika wema na ucha Mungu. Na katika kinachonasibiana na hali hii ni kwamba wanandoa wanapotengana wakati wa eda, hasa ikiwa mtoto amezaliwa kati yao, mara nyingi hutokea migogoro na ugomvi juu ya matunzo ya mke huyu na mtoto kwa sababu ya chuki iliyoko kati yao, kwa hivyo mambo mengi yanaathiriwa na hayo. Basi kila mmoja wao anafaa kushauri kwa wema na kuishi kwa uzuri, siyo kugombana kupingana au kugombana. "Na mkiona uzito kati yenu" ikiwa wanandoa hao hawatakubaliana juu ya kumnyonyesha mtoto wake, "basi amnyonyeshee mwanamke mwengine" asiyekuwa yeye, "wala hapana ubaya kwenu mkitoa mlichoahidi kwa mujibu wa ada." Hili ni pale mtoto anakubali kunyonya mtu asiyekuwa mama yake. Lakini ikiwa hakubali isipokuwa titi la mama yake, basi mama yake tu ndiye atakayemnyonyesha, na itamlazimu kufanya hivyo ikiwa atakataa, na atastahiki ujira mfano wa ule wanaopewa mfano wake ikiwa hawakuwa hawatakubaliana juu ya ujira maalumu. Hili limechukuliwa kutoka katika Aya hii tukufu kulingana na maana yake. Kwa maana, mtoto alipokuwa tumboni mwa mama yake kwa kipindi chote cha ujauzito, hakukuwa na njia ya kutoka humo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akamuamrisha mlinzi wake kumpa matumizi ya kila siku. Basi pale alipozaliwa na kukawa na uwezekano wa kunyonyeshwa na mama yake au na wengineo, Mwenyezi Mungu Mtukufu akaruhusu mambo yote hayo mawili. Basi ikiwa yuko katika hali ambayo hawezi kunyonyeshwa isipokuwa na mama yake tu, basi hilo linakuwa sawa na wakati alivyokuwa tumboni, na mama yake anakuwa ndiye peke yake anayeweza kumnyonyesha.