الطلاق
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلَّـٰٓـِٔى يَئِسْنَ مِنَ ٱلْمَحِيضِ مِن نِّسَآئِكُمْ إِنِ ٱرْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَـٰثَةُ أَشْهُرٍ وَٱلَّـٰٓـِٔى لَمْ يَحِضْنَ ۚ وَأُو۟لَـٰتُ ٱلْأَحْمَالِ أَجَلُهُنَّ أَن يَضَعْنَ حَمْلَهُنَّ ۚ وَمَن يَتَّقِ ٱللَّهَ يَجْعَل لَّهُۥ مِنْ أَمْرِهِۦ يُسْرًا ٤
{4} Mwenyezi Mungu Mtukufu alipotaja kuwa talaka sahihi iliyoamrishwa ni ile ambayo wanawake wanaweza kuanza eda yao, akataja eda, na akasema: "Na wale waliosita hedhi miongoni mwa wanawake wenu." Yaani, wale waliokuwa wakipata hedhi, kisha hedhi yao ikakatika kwa sababu ya uzee au kitu kingine, na hakuna matumaini ya kurudi kwake. Basi eda yao ni miezi mitatu, kila mwezi inapaswa kuchukuliwa kuwa ni hedhi moja. "Pamoja na ambao hawapati hedhi." Yaani, wasichana wadogo ambao bado hawajapata hedhi, au wanawake watu wazima ambao hawajapata hedhi kabisa. Hao ni kama wanawake walioacha kupata hedhi, eda yao ni miezi mitatu. Ama wale wanaopata hedhi, basi Mwenyezi Mungu akataja eda yao katika kauli yake: "Na wanawake walioachwa kwa talaka wangoje peke yao mpaka tahara (au hedhi) tatu zipite." Na kauli yake: "Na wenye mimba, eda yao mpaka watakapozaa" vyote vilivyomo matumboni mwao, kiwe kimoja au vingi, na hapo haitazingatiwa miezi au kitu chochote kile. "Na anayemcha Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humfanyia mambo yake kuwa mepesi."