انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الجمعة
السورة ٦٢

الجمعة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِذَا نُودِىَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوْمِ ٱلْجُمُعَةِ فَٱسْعَوْا۟ إِلَىٰ ذِكْرِ ٱللَّهِ وَذَرُوا۟ ٱلْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ ٩

{9} Mwenyezi Mungu Mtukufu anawaamrisha waja wake waumini kuhudhuria Sala ya Ijumaa na kuifanyia hima kila iitwapo na kujitahidi kuifikia na kuipa muhimu mkubwa, wala haikumaanishwa kuikimbilia ambako kumekatazwa wakati wa kuiendea swala. Na kauli yake: "Na wacheni biashara." Yaani, acheni kuuza na kununua inapoitwa kwa ajili ya swala na muiendee. Kwani "hayo ni bora kwenu" kuliko kujishughulisha kwenu na kuuza na kununua, au kukosa Swala ya faradhi, ambayo ni miongoni mwa faradhi ya lazima zaidi. "Lau kama mnajua" kwamba kilichoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora na ni cha kudumu zaidi, na kwamba anayeipendelea dunia hii kuliko akhera, basi hakika amehasiri hasara ya uhakika, ilhali yeye alifikiria kwamba amepata faida.