الصف
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَأُخْرَىٰ تُحِبُّونَهَا ۖ نَصْرٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ ۗ وَبَشِّرِ ٱلْمُؤْمِنِينَ ١٣
{13} Ama malipo ya kidunia kwa biashara hii, basi aliyataja katika kauli yake: “Na kinginecho mkipendacho” Yaani, na mtapata kitu kingine mnachokipenda, nacho ni: “nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu” dhidi ya maadui zenu, ambayo kwayo mtapata utukufu na furaha, “na ushindi ulio karibu” ambao kwao duara la Uislamu litapanuka, na ambao kwao mtapata riziki ya kunjufu. Haya ndiyo malipo ya waumini wanaopambana katika jihadi. Na ama waumini wasio watu wa kufanya jihadi, wenzao wanapofanya jihadi, Mwenyezi Mungu hakuwakunjulia katika fadhila zake na wema wake. Bali alisema: “Na wabashirieni Waumini” kwa malipo ya haraka na ya baada ya muda mrefu. Kila mmoja kulingana na imani yake, hata wasipofikia daraja ya wale wanaopambana katika jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu. Kama alivyosema Nabii – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie: “Mwenye kumridhia Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola Mlezi, na Uislamu kuwa ndiyo dini, na Muhammad kuwa ndiye Mtume, atakuwa amestahiki kuingia katika bustani za mbinguni.” Abu Said Al-Khudri, msimuliaji wa Hadithi hii, alistaajabishwa na hilo na akasema: ‘Irudie niisikie tena ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu!’ Kwa hivyo akamrudilia tena, kisha akasema: “Na nyingine ambayo kwayo mja atanyanyuliwa ngazi mia moja katika bustani za mbinguni, na umbali uliopo baina ya kila ngazi mbili ni kama umbali uliopo baina ya mbingu na ardhi.’ Akasema: ‘Ni nini hilo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Akasema: Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu. Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.’ Imepokelewa na Muslim.