انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الممتحنة
السورة ٦٠

الممتحنة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩

إِنَّمَا يَنْهَىٰكُمُ ٱللَّهُ عَنِ ٱلَّذِينَ قَـٰتَلُوكُمْ فِى ٱلدِّينِ وَأَخْرَجُوكُم مِّن دِيَـٰرِكُمْ وَظَـٰهَرُوا۟ عَلَىٰٓ إِخْرَاجِكُمْ أَن تَوَلَّوْهُمْ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُمْ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ ٩

{9} Na kauli yake: “Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki wa kusaidiana nao, na wale waliokupigeni vita kwa sababu ya dini” na kwa sababu ya kuifanyia uadui Dini ya Mwenyezi Mungu na wale wanaoisimamisha, “na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia” na watu wengine “katika kufukuzwa kwenu.” Mwenyezi Mungu amekukatazeni kuwafanya marafiki wa kusaidiana nao na kwa mapenzi kwa kauli na vitendo. Ama kuwafanyia kwenu wema bila ya kuwafanya marafiki wendani washirikina, basi Mwenyezi Mungu hakukukatazeni hayo, bali hayo yamo katika amri ya jumla ya kuwafanyia wema jamaa na wanadamu wengineo, “Na wanaowafanya hao marafiki wendani” miongoni mwenu “basi hao ndio madhalimu.” Dhuluma hii inakuwa kulingana na kiasi cha kuwafanya marafiki. Na kama ni kuwafanya marafiki wendani kikamilifu, basi hilo linakuwa ukafiri unaotoa nje ya duara la Uislamu, na chini ya hapo kuna viwango vingine ambavyo ni vikubwa na vingine viko chini ya hapo.