الممتحنة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَوَلَّوْا۟ قَوْمًا غَضِبَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ قَدْ يَئِسُوا۟ مِنَ ٱلْـَٔاخِرَةِ كَمَا يَئِسَ ٱلْكُفَّارُ مِنْ أَصْحَـٰبِ ٱلْقُبُورِ ١٣
{13} Yaani, enyi Waumini, ikiwa mnamuamini Mola wenu Mlezi, na mnafuata radhi zake, na mnaepuka ghadhabu yake, “Msiwafanye rafiki wa kusaidiana nao katika watu ambao Mwenyezi Mungu amewakasirikia.” Kwani, aliwakasirikia kwa sababu ya ukafiri wao, na hili linajumuisha kila aina ya makafiri, “Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera.” Yaani, wamenyimwa heri ya Akhera, kwa hivyo huko hawana fungu lolote. Basi jihadharini msije mkawa marafiki wendani wao mkaja mkakubaliana nao katika uovu wao na ushirikina wao, kwa hivyo mkanyimwa heri ya Akhera kama walivyonyimwa wao. Na kauli yake: “kama makafiri walivyowakatia tamaa watu wa makaburini” walipofika Akhera na wakaona ukweli wa jambo hilo, na wakajua kwa yakini kwamba wao hawana fungu huko. Inawezekana kwamba maana ya “Hao wamekwisha kata tamaa ya Akhera” ni kuwa waliikataa na wakaikufuru. Kwa hivyo haliwi jambo la kushangaza kwamba wanakimbilia katika mambo anayoyachukia Mwenyezi Mungu na mambo yenye kusababisha adhabu yake, na kwamba walikata tamaa na maisha ya akhera kama vile makafiri hapa duniani wanaokanusha kufufuliwa walivyokata tamaa ya kurudi kwa watu wa makaburini kwa Mwenyezi Mungu.
Imekamilika tafsiri ya sura hii, na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye zaidi.