انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٩٧

وَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَ لَكُمُ ٱلنُّجُومَ لِتَهْتَدُوا۟ بِهَا فِى ظُلُمَـٰتِ ٱلْبَرِّ وَٱلْبَحْرِ ۗ قَدْ فَصَّلْنَا ٱلْـَٔايَـٰتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ٩٧

{97} "Na Yeye ndiye aliyewawekea nyota ili mwongoke kwazo katika giza mbalimbali ya bara na bahari} wakati njia zinapowachanganya, na anapochanganyikiwa mwenye kupitia hapo. Kwa hivyo Mwenyezi Mungu akazifanya nyota kuwa mwongozo kwa viumbe kuiendea njia wanayoihitaji kuifuata kwa sababu ya maslahi yao, na biashara zao, na safari zao. Miongoni mwake kuna nyota ambazo haziachi kuonekana, wala hazisongi kutoka pahali pake. Na kuna zile zinazoendelea kusonga, ambazo wanajua kusonga kwake watu wa elimu ya hayo, na wanajua kwazo mielekeo na nyakati. Na Aya hii na nyinginezo mfano wake zilionyesha kuruhusiwa kujifunza mwendo wa sayari na masimamo yake, ambayo inaitwa sayansi ya miendo. Kwa maana mwongozo hauwezi kutimia wala hauwezekani isipokuwa kwa njia hii. "Hakika tumezieleza kwa kina Ishara hizi," yaani,tumezibainisha, na kuziweka wazi, na kuzipambanua kila sampuli na aina katika hizo kutoka kwa nyingine, kwa kiasi kwamba zikawa Aya za Mwenyezi Mungu ni wazi na dhahiri "kwa kaumu wanaojua;" yaani, kwa watu wa elimu na maarifa. Kwa maana hao ndio ambao wanaoongeleshwa, na wanaotakiwa kuitikia. Tofauti na watu wa ujinga na ugumu wanaozipa mgongo Aya za Mwenyezi Mungu, na elimu ambayo walikuja nayo Mitume. Basi ubainisho huu hauwanufaishi kitu, na kueleza kwa kina hakuwaondolei chenye kuwachanganya, na kuweka wazi hakuwaondolei tatizo lolote.