الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَلَوْ جَعَلْنَـٰهُ مَلَكًا لَّجَعَلْنَـٰهُ رَجُلًا وَلَلَبَسْنَا عَلَيْهِم مَّا يَلْبِسُونَ ٩
{9} Na pamoja na hayo, ikiwa Malaika angeteremshwa kwao, hawangeweza kupokea kutoka kwake, wala hawangeweza kustahimili hilo, wala uwezo wao unaoisha haungeweza hilo. "Na kama tungelimfanya Malaika, bila ya shaka tungelimfanya kuwa mwanamume" kwa sababu hekima haitaki isipokuwa hilo; "na tungeliwatilia matatizo yale wanayoyatatiza wao." Yaani, jambo hilo lingeliwachanganya, na hilo ni kwa sababu walivyojichanganya wenyewe. Kwa maana Walijenga mambo yao juu ya kanuni hii ambayo ina mkanganyiko na kutobainisha haki. Na haki ilipowajia kwa njia zake sahihi na kanuni zake, ambazo ndizo kanuni zake halisi, hilo halikuweza kuwaongoa huku wengine wakiongoka kwalo. Na dhambi ni yao wenyewe kwa sababu walijifungia wenyewe milango ya uwongofu na wakajifungulia milango ya upotovu.