انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٣

وَتِلْكَ حُجَّتُنَآ ءَاتَيْنَـٰهَآ إِبْرَٰهِيمَ عَلَىٰ قَوْمِهِۦ ۚ نَرْفَعُ دَرَجَـٰتٍ مَّن نَّشَآءُ ۗ إِنَّ رَبَّكَ حَكِيمٌ عَلِيمٌ ٨٣

{83} Na alipohukumu kwa ajili ya Ibrahim, amani iwe juu yake, kwa yale aliyobainisha kwayo miongoni mwa hoja za mkato. Akasema, "Na hizo ndizo hoja zetu tulizompa Ibrahim dhidi ya kaumu yake; yaani, aliinuka kwazo juu yao, na akawashinda kwazo. "Tunamnyanyua tumtakaye daraja mbalimbali" kama tulivyonyanyua daraja za Ibrahim, amani iwe juu yake katika dunia na Akhera. Kwa maana, kwa elimu, mwenyezi Mungu humpandisha daraja mbalimbali mwenyewe juu ya waja wake, hasa mwenye elimu anayeifanyia kazi, anayeifunza wengine. Yeye Mwenyezi Mungu humfanya kuwa imamu kwa watu kulingana na hali yake. Matendo yake yanatukuzwa, na nyayo zake zinafuatwa, na nuru yake inatumika kuangazia, na inatembewa kwa elimu yake katika giza la mazingira yake. Yeye Mtukufu amesema, "Mwenyezi Mungu huwainua wale walioamini miongoni mwenu, na wale waliopewa elimu daraja mbalimbali." "Hakika Mola Mlezi wako ni Mwenye hekima kubwa, Mwenye kujua yote," kwa hivyo, haiweki elimu na hekima isipokuwa katika mahali pake vinapostahiki, naye ndiye Anayepajua zaidi pahali hapa, na panavyopaswa kuwa.