الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ هُوَ ٱلْقَادِرُ عَلَىٰٓ أَن يَبْعَثَ عَلَيْكُمْ عَذَابًا مِّن فَوْقِكُمْ أَوْ مِن تَحْتِ أَرْجُلِكُمْ أَوْ يَلْبِسَكُمْ شِيَعًا وَيُذِيقَ بَعْضَكُم بَأْسَ بَعْضٍ ۗ ٱنظُرْ كَيْفَ نُصَرِّفُ ٱلْـَٔايَـٰتِ لَعَلَّهُمْ يَفْقَهُونَ ٦٥
{65} Yaani, Yeye Mwenyezi ni Muweza wa kuwatumia adhabu kutokea kila upande, "kutoka juu yenu au kutoka chini ya miguu yenu, au awavishe fujo." Yaani, Awachanganye "fujo la mfarakano, na awaonjeshe baadhi yenu jeuri ya wenzi wenu." Yaani, katika majaribio na kuuana wenyewe kwa wenyewe. Basi yeye ni muweza wa yote hayo. Basi jihadhari na kudumu katika kumuasi, ikaja kuwapata adhabu itakayowangamiza na kuwafutilia mbali. Na pamoja na hili, akasema kwamba Yeye ni Muweza wa hayo, lakini katika rehema Zake ni kwamba Aliwaondolea Ummah huu adhabu kutokea juu yao kwa kupigwa kwa mawe, na changarawe, na mfano wake, na kutokea chini ya miguu yao kwa kudidimizwa. Lakini aliwaadhibu baadhi ya wale aliowaadhibu miongoni mwao kwa kuwaonjesha baadhi yao jeuri ya baadhi yao, na akawapa baadhi yao mamlaka juu ya wenzi wao kwa adhabu hizi zilizotajwa, kama adhabu ya haraka ambayo wataiona wenye kuzingatia na wanaoifanyia kazi wataihisi. "Tazama vipi tunavyozieleza Aya;" yaani, tunavyozitofautisha na kuzileta kwa namna nyingi, na zote zinaonyesha haki, "ili wafahamu." Yaani, wafahamu kile walichoumbwa kwa ajili yake na waelewe uhakika wa kisheria na matakwa ya kimungu.