انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥١

وَأَنذِرْ بِهِ ٱلَّذِينَ يَخَافُونَ أَن يُحْشَرُوٓا۟ إِلَىٰ رَبِّهِمْ ۙ لَيْسَ لَهُم مِّن دُونِهِۦ وَلِىٌّ وَلَا شَفِيعٌ لَّعَلَّهُمْ يَتَّقُونَ ٥١

{51} Qur’ani hii ni onyo kwa viumbe wote, lakini wanafaidika nayo tu; "wale wanaohofu kuwa watakusanywa kwa Mola wao Mlezi." Basi wao wana yakini ya kuondoka kutoka kwenye Nyumba hii hadi kwenye nyumba ya kudumu. Ndiyo maana wanachukua pamoja nao yale yatakayowanufaisha na wanayaacha yale ambayo yatawadhuru. "Hawana kando naye"; yaani, kando na Mwenyezi Mungu, "msimamizi wala mwombezi." Yaani, hakuna wa kuwasimamia mambo yao ili wapate wanayoyataka, na kuwazuia kutokana na yale wanayoyatahadhari, wala hakuna wa kuwaombea. Kwa sababu viumbe wote hawana kitu chochote katika jambo hilo. "Ili wamche Mwenyezi Mungu" kwa kutekeleza amri zake na kuepuka makatazo yake. Kwa maana onyo linasababisha hayo, na ni sababu miongoni mwa sababu zake.