الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
بَلْ إِيَّاهُ تَدْعُونَ فَيَكْشِفُ مَا تَدْعُونَ إِلَيْهِ إِن شَآءَ وَتَنسَوْنَ مَا تُشْرِكُونَ ٤١
{41} "Bali Yeye ndiye mtakayemuomba, naye atawaondolea mnachomwombea akipenda. Na mtasahau hao mnaowafanya washirika wake." Basi ikiwa hii ndiyo hali yenu pamoja na wenza wenu hawa katika nyakati za shida, mnawasahau kwa sababu mnajua kwamba wao hawawamilikii kudhuru, wala kunufaisha, wala mauti, wala uhai, wala kufufua, na mnamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake dua Kwa sababu mnajua kwamba Yeye tu ndiye mwenye kudhuru, mwenye kunufaisha, mwenye kuitikia maombi ya mwenye haja kubwa. Basi mna nini katika hali nzuri mnamshirikisha na mnamfanyia washirika? Je, iliwaonyesha hilo akili au andiko? Au mna mamlaka yoyote juu ya hili? Au mnamzulia Mwenyezi Mungu uongo?