الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِى ٱلظُّلُمَـٰتِ ۗ مَن يَشَإِ ٱللَّهُ يُضْلِلْهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ ٣٩
{39} Haya ni kubainisha hali ya wale waliokadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu, na waliowakadhibisha Mitume wake, kwamba wao wenyewe walijifungia mlango wa uwongofu, na wakajifungulia mlango wa maangamivu; na kwamba wao ni "viziwi" wasioisikia haki, "mabubu" wasioweza kuizungumza. Basi hawazungumzi isipokuwa batili "wamo katika giza mbalimbali". Yaani, walitumbukia katika giza mbalimbali la ujinga, na ukafiri, na dhulma, na ukaidi, na maasia; na haya ni katika Mwenyezi Mungu kuwapoteza. Basi yule ambaye "Mwenyezi Mungu anataka, anampoteza, na yule ambaye anataka, anamuweka katika Njia iliyonyooka." Kwa sababu ni Yeye pekee wa kuongoza na kupotosha kulingana na inavyotaka neema yake na hekima yake.