الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ إِنَّ صَلَاتِى وَنُسُكِى وَمَحْيَاىَ وَمَمَاتِى لِلَّهِ رَبِّ ٱلْعَـٰلَمِينَ ١٦٢
{162} Kisha akateua kutoka katika hayo ibada tukufu zaidi, akasema, "Sema: Hakika Swala yangu, na kuchinja kwangu." Na hiyo ni kutokana na utukufu wa ibada hizi mbili na fadhila zake, na kuonyesha kwake ya kumpenda Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumfanyia yeye tu dini, na kujikurubisha Kwake kwa moyo, na ulimi na viungo, na kwa kuchinja, ambako ni kutoa kile ambacho nafsi inakipenda kutoka katika mali kwa ajili ya yule aliye mpendwa zaidi kwake, ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu na mwenye kumfanyia Mwenyezi Mungu peke yake swala yake na kuchinja kwake, hayo yatamlazimu kumfanyia yeye tu katika matendo yake mengineyo yote. Na kauli yake, "Na uhai wangu, na kufa kwangu;" yaani, ninayoyafanya katika uhai wangu, na yale anayonipitishia Mwenyezi Mungu, na yale anayoniandikia katika kufa kwangu; yote hayo “ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu.”