الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ هَلُمَّ شُهَدَآءَكُمُ ٱلَّذِينَ يَشْهَدُونَ أَنَّ ٱللَّهَ حَرَّمَ هَـٰذَا ۖ فَإِن شَهِدُوا۟ فَلَا تَشْهَدْ مَعَهُمْ ۚ وَلَا تَتَّبِعْ أَهْوَآءَ ٱلَّذِينَ كَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَا وَٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ وَهُم بِرَبِّهِمْ يَعْدِلُونَ ١٥٠
{150} Yaani, mwambie yule aliyeyaharamisha yale aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu na akayanasibisha hayo kwa Mwenyezi Mungu: Waleteni mashahidi wenu ambao wanashuhudia kwamba Mwenyezi Mungu ameyaharamisha haya! Na wakiambiwa maneno haya, basi wako baina ya mambo mawili: Ima wasimlete yeyote kushuhudia haya, basi madai yao yakawa ni batili, yasiyokuwa na mashahidi na ushahidi. Na ima wamlete yeyote anayewashuhudia hilo. Na hakuna anayaweza kushuhudia hayo isipokuwa kila mwongo mkubwa mwenye dhambi asiyekubaliwa ushahidi wake. Na hili si katika mambo ambayo inaruhusika kwa waadilifu kuyashuhudia. Na ndiyo maana Akasema yeye Mtukufu, akimkataza Nabii wake na wafuasi wake ushahidi huu: "Kwa hivyo, wakishuhudia, basi wewe usishuhudie pamoja nao. Wala usifuate matamanio ya wale waliozikadhibisha Ishara zetu, na ambao hawaamini katika Akhera, nao wanamlinganisha Mola wao Mlezi na wengine." Yaani, wanawafanya wengine kuwa sawa na Yeye miongoni mwa wenza, na viabudiwavyo vyote. Na ikiwa waliikufuru Siku ya Mwisho na hawampwekeshi Mwenyezi Mungu, matamanio yao yanakuwa yenye kuafikiana na itikadi zao, na yanakuwa yenye kuzunguka baina ya ushirikina na ukadhibishaji wa haki. Kwa hivyo ikafaa zaidi kwa matamanio ambayo hii ndiyo hali yake kwamba Mwenyezi Mungu awakataze walio bora zaidi wa viumbe vyake kuyafuata, na kushuhudia pamoja na mabwana wake, na ikajulikana hapo kwamba kuharamisha kwao yale ambayo Mwenyezi Mungu alihalalisha kulitokana na matamanio hayo potofu.