الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل رَّبُّكُمْ ذُو رَحْمَةٍ وَٰسِعَةٍ وَلَا يُرَدُّ بَأْسُهُۥ عَنِ ٱلْقَوْمِ ٱلْمُجْرِمِينَ ١٤٧
{147} Yaani, ikiwa washirikina hawa watakukadhibisha, basi endelea kuwalingania kwa kuwatia moyo na kuwatishia, na waambie kwamba Mwenyezi Mungu ni "Mwenye rehema iliyoenea." Yaani, ya jumla na yenye kuingia ndani yake viumbe vyote. Basi ikimbilieni rehema yake kwa sababu zake, ambazo kichwa chake, na msingi wake, na kiini chake ni kumsadiki Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – katika yale aliyokuja nayo. "Wala haizuiwi adhabu yake kwa kaumu wahalifu." Yaani, wale ambao uhalifu wao ni mwingi, na dhambi zao. Basi jihadharini na uhalifu mbalimbali unaofikisha kwenye adhabu ya Mwenyezi Mungu, ambayo kubwa zaidi yake na kichwa chake ni kumkadhibisha Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake.