الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ أَغَيْرَ ٱللَّهِ أَتَّخِذُ وَلِيًّا فَاطِرِ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَهُوَ يُطْعِمُ وَلَا يُطْعَمُ ۗ قُلْ إِنِّىٓ أُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ أَوَّلَ مَنْ أَسْلَمَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ ١٤
{14} "Sema," uwaambie hawa wanaomshirikisha Mwenyezi Mungu, "nimfanye rafiki mwandani asiyekuwa Mwenyezi Mungu," katika viumbe hawa wasiojiweza ili wanipe ulinzi na kunisaidia? Basi simchukui asiyekuwa Yeye, Mtukufu kuwa rafiki mwandani. Kwa sababu Yeye "ndiye Muumba mwanzilishi wa mbingu na ardhi;" yaani, Muumba wake na Mwendeshaji wake, "naye ndiye anayelisha wala halishwi?" Yaani, Yeye ndiye Mwenye kuwaruzuku viumbe vyote bila ya Yeye kuwa na haja yoyote kutoka kwao. Basi vipi inafaa kwangu kumchukua rafiki mlinzi asiyekuwa Yeye Muumba, mwenye kuruzuku, mwenye kujitosheleza, Msifiwa? "Sema: Hakika Mimi nimeamrishwa kwamba niwe wa kwanza wa wenye kusilimu;" kwa Mwenyezi Mungu kwa tauhidi na kumfuata kwa utiifu. Kwa sababu mimi ninastahiki zaidi kuliko wengine yeyote kufuata amri za Mola wangu Mlezi, "Na wala kabisa usiwe miongoni wa washirikina." Yaani, pia nimekatazwa kuwa miongoni mwa washirikina. Si katika itikadi yao, wala katika kukaa nao, wala katika kukusanyika nao. Na hili ndiyo faradhi ya lazima kwangu, na wajibu wa lazima kwangu.