الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
يَـٰمَعْشَرَ ٱلْجِنِّ وَٱلْإِنسِ أَلَمْ يَأْتِكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ ءَايَـٰتِى وَيُنذِرُونَكُمْ لِقَآءَ يَوْمِكُمْ هَـٰذَا ۚ قَالُوا۟ شَهِدْنَا عَلَىٰٓ أَنفُسِنَا ۖ وَغَرَّتْهُمُ ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا وَشَهِدُوا۟ عَلَىٰٓ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا۟ كَـٰفِرِينَ ١٣٠ ذَٰلِكَ أَن لَّمْ يَكُن رَّبُّكَ مُهْلِكَ ٱلْقُرَىٰ بِظُلْمٍ وَأَهْلُهَا غَـٰفِلُونَ ١٣١
{130} Kisha Mwenyezi Mungu akawakemea wote wale walioipa mgongo haki na wakaikataa miongoni mwa majini na watu, na akabainisha makaosa yao, kwa hivyo wakakiri hilo. Akasema, "Enyi kundi la majini na watu! Je, hawakuwajia Mitume kutokana na nyinyi wenyewe wakiwabainishia Aya zangu," zilizo wazi na bainifu, ambazo ndani yake kuna maelezo ya kina ya maamrisho na makatazo, na heri na shari, na ahadi nzuri na ahadi ya adhabu; "Na wakiwasimulia kukutana na Siku yenu hii?" Na wanawafunza kuwa kunusurika ndani yake na kufuzu ni kwa kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake, na kwamba mashaka na hasara ni katika kuyapoteza hayo. Kwa hivyo, wakakiri hilo na wakakubali, na wakasema, "Tumeshuhudia juu ya nafsi zetu. Na yaliwadanganya maisha ya dunia;" kwa mapambo yake, na merembesho yake, na neema yake; kwa hivyo, wakatulia na kuridhika navyo, lakini vikawashughulisha na maisha ya akhera. "Nao watajishuhudia wenyewe ya kwamba walikuwa makafiri." Basi hoja ya Mwenyezi Mungu ikasimama juu yao, na wakati huo kila mmoja wao akajua kwamba hata wao wenyewe uadilifu wa Mwenyezi Mungu juu yao. [Basi akawaambia kwa kuwahukumu kwa adhabu chungu: Ingieni katika kundi la umma uliopita kabla yenu miongoni mwa majini na watu. Walifanya kama mliyoyafanya, na wakafurahia kwa fungu lao kama mlivyofurahia, na wakazama katika batili kama mlivyozama. Wao kwa hakika walikuwa wenye hasara. Yaani, wa mwanzo katika hawa na wa mwisho. Na ni hasara gani iliyo kubwa zaidi kuliko kuzipoteza bustani za neema na kunyimwa kuwa karibu na Mkarimu zaidi wa wakarimu?]