الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
لَهُمْ دَارُ ٱلسَّلَـٰمِ عِندَ رَبِّهِمْ ۖ وَهُوَ وَلِيُّهُم بِمَا كَانُوا۟ يَعْمَلُونَ ١٢٧
127. Na ndiyo maana akasema, "Hao watapata nyumba ya salama kwa Mola Mlezi wao." Na Pepo iliitwa nyumba ya amani kwa sababu ya usalama wake kutokana na kila dosari, na maradhi, na machafu, na wasiwasi, dhiki na yasiyokuwa hayo miongoni mwa yale yanayokera. Na inalazimu kutokana na hilo kwamba furaha yake ni kamilifu sana na timilifu zaidi, kiasi kwamba hawawezi kuieleza wenye kueleza, na wala wenye kutamani hawatamani zaidi yake, miongoni mwa raha ya nafsi, na moyo na mwili. Na watakuwa ndani yake na yale yanayotamaniwa na nafsi na yale yanayopendeza macho, nao watadumu humo. "Naye ndiye Rafiki Mlinzi wao" ambaye amesimamia kuwaendesha, na kuwalea, na akawafanyia upole katika mambo yao yote, na akawasaidia katika kumtii Yeye, na akawasahilishia kila sababu inayofikisha kwenye mapenzi yake. Na aliwasimamia kwa sababu ya matendo yao mema na yale waliyotanguliza walikusudia kwayo ridhaa ya Mola wao Mlezi. Tofauti na yule aliyempa mgongo Mola wake Mlezi na akafuata matamanio yake, basi huyo alipewa Shetani mamlaka juu yake, kwa hivyo akamsimamia, na akamharibia dini yake na dunia yake.