انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١٧

إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ مَن يَضِلُّ عَن سَبِيلِهِۦ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ ١١٧

{117} Na yule ambaye ni namna hii, basi mwenyezi Mungu anafaa zaidi kuwaonya waja wake kuhusiana naye, na awaeleze hali zake. Kwa sababu hata kama haya anaambiwa Nabii -rehema na amani ziwe juu yake, - Ummah wake wanachukua kiigizo kwake katika hukumu zote ambazo si maalumu kwake tu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye mkweli zaidi wa usemi, na mkweli zaidi wa maneno. Na "ndiye Anayejua vyema yule aliyepotea Njia yake," naye ndiye anayejua vyema anayeongoka, na wa kumuongoa. Kwa hivyo, enyi Waumini, ni lazima mfuate nasaha zake, na amri zake, na makatazo yake. Kwa sababu Yeye ndiye anayejua zaidi masilahi yenu, na mwenye rehema zaidi kwenu kuliko nyinyi wenyewe kwa nafsi zenu. Na Aya hii iliashiria kwamba idadi kubwa ya watu wanaofuata jambo haionyeshi kuwa ndiyo haki, wala idadi ndogo ya watu wanaofuata jambo haionyeshi kuwa si haki. Bali uhakika wa mambo uko kinyume cha hayo. Kwa kuwa Watu wa haki ndio wachache zaidi kwa idadi, na ndio wakubwa wa cheo na malipo kwa Mwenyezi Mungu. Bali, kinachotakiwa ni kutumia njia zinazofikisha kwa haki au batili kuwa ndizo ushahidi wake.