انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١١

وَلَوْ أَنَّنَا نَزَّلْنَآ إِلَيْهِمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةَ وَكَلَّمَهُمُ ٱلْمَوْتَىٰ وَحَشَرْنَا عَلَيْهِمْ كُلَّ شَىْءٍ قُبُلًا مَّا كَانُوا۟ لِيُؤْمِنُوٓا۟ إِلَّآ أَن يَشَآءَ ٱللَّهُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ يَجْهَلُونَ ١١١

{111} Na vivyo hivyo, kuifungamanisha imani na kutaka kwao na mapenzi yao peke yao, na kutomtegemea mwenyezi Mungu, ni miongoni mwa makosa makubwa zaidi. Kwa maana, lau zingewajia Ishara kubwa kama vile kuwateremshia Malaika wakimshuhudia Mtume ujumbe, na kuwaongelesha wafu, na kuwafufua baada ya kufa kwao. Na tukawakusanyia kila kitu ili kiwaongeleshe mbele yao, kwa kuviona, na kwa moja kwa moja vikishuhudia ukweli wa yale aliyokuja nayo Mtume; basi hawangepata imani kama mwenyezi Mungu hangetaka waamini, lakini wengi wao wanafanya ujinga. Ndiyo maana wakafungamanisha kuamini kwao na kuja kwa Aya tu. lakini akili na elimu ni kwamba mja awe lengo lake ni kufuata haki, na aitafute kwa njia ambazo Mwenyezi Mungu alizibainisha, na azitendee kazi, amuombe msaada Mola wake Mlezi katika kuifuata, na wala asijitegemee nafsi yake na uwezo wake na nguvu zake, na wala asitafute katika Aya anazopendekeza yeye, zisizokuwa na faida yoyote.