انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الأنعام
السورة ٦

الأنعام

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآيات ١٠٤–١٠٧

قَدْ جَآءَكُم بَصَآئِرُ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنْ أَبْصَرَ فَلِنَفْسِهِۦ ۖ وَمَنْ عَمِىَ فَعَلَيْهَا ۚ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيْكُم بِحَفِيظٍ ١٠٤ وَكَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ ٱلْـَٔايَـٰتِ وَلِيَقُولُوا۟ دَرَسْتَ وَلِنُبَيِّنَهُۥ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ ١٠٥ ٱتَّبِعْ مَآ أُوحِىَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ ۖ لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ وَأَعْرِضْ عَنِ ٱلْمُشْرِكِينَ ١٠٦ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَآ أَشْرَكُوا۟ ۗ وَمَا جَعَلْنَـٰكَ عَلَيْهِمْ حَفِيظًا ۖ وَمَآ أَنتَ عَلَيْهِم بِوَكِيلٍ ١٠٧

{104} "Hakika zimekwisha wajia hoja wazi wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo, mwenye kuziona, basi ni kwa faida yake mwenyewe. Na mwenye kupofuka, basi ni hasara yake. Nami si mtunzaji wenu." Kwa sababu ya yale aliyoyabainisha Yeye Mtukufu miongoni mwa Aya mbalimbali zilizo wazi, na ushahidi ulio wazi, unaoashiria kwenye haki katika matakwa yote na makusudio yote. Akawatanabahisha waja juu yake, na akajulisha kuwa uwongofu wao na kinyume chake ni juu yao wenyewe, kwa hivyo akasema; "Hakika zimekwisha wajia hoja wazi wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi." Yaani, Aya mbalimbali zinazobainisha haki na kuuwekea moyo iwe wazi kama jua linavyokuwa kwa macho. Kwa sababu yaliyo ndani yake ya ufasaha wa matamshi, na ubainifu wake, na uwazi wake, na kulingana kwake na maana tukufu na hakika nzuri nzuri. Kwa sababu zinatoka kwa Mola Mlezi, ambaye aliwalea viumbe wake kwa kila aina ya neema zake za dhahiri na zilizofichika, ambazo katika bora zake zaidi na tukufu zaidi ni ubainifu wa Aya mbalimbali na kuweka wazi wa matatizo. "Kwa hivyo, mwenye kuona," kwa Aya hizo sehemu za mazingatio na anafanya matendo kulingana na matakwa yake, "basi ni kwa faida yake mwenyewe" kwa maana Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitegemea, Msifiwa. Na mwenye kupofuka kwa kuonyeshwa, naye akaacha kuona, na akakemewa, lakini hakukemeka, na akabainishiwa haki, lakini hakuifuata wala kuinyenyekea. Basi upofu wake madhara yake ni juu yake. "Wala mimi" Ewe Mtume "si mtunzaji wenu wenu." Nikihifadhi vitendo vyenu na kuviangalia kila wakati. Lakini lililo juu yangu ni kufikisha kuliko wazi, na tayari nilikwisha tekeleza hilo, na nikafikisha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwangu. Basi hii ndiyo kazi yangu, na zaidi ya hilo, mimi sikupewa kazi hiyo.