انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحشر
السورة ٥٩

الحشر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥

مَا قَطَعْتُم مِّن لِّينَةٍ أَوْ تَرَكْتُمُوهَا قَآئِمَةً عَلَىٰٓ أُصُولِهَا فَبِإِذْنِ ٱللَّهِ وَلِيُخْزِىَ ٱلْفَـٰسِقِينَ ٥

Na wakati Banu Nadhir walipomlaumu Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - na Waislamu kuhusiana na kukata kwao mitende na miti, na wakadai kwamba hilo ni kufanya uharibifu na wakatumia hilo kuwakashifu Waislamu, Mwenyezi Mungu Mtukufu akajulisha kwamba kukata mitende hiyo ikiwa waliikata au kuiwacha imesimama ikiwa waliiacha, ni kwa idhini yake na amri yake, “ili awahizi wavukao mipaka,” ambapo aliwawezesha kukata mitende yao na kuichoma; ili hilo liwe ni adhabu kwao na fedheha duniani na udhalilifu utakaoonyesha kutoweza kwao kitu kabisa, kwa kuwa hawakuweza kuokoa mitende yao ambayo ni chanzo cha chakula chao kikuu. Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa hali ya Banu Nadhir na jinsi Mwenyezi Mungu [Mtukufu] alivyowaadhibu duniani.