انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحشر
السورة ٥٩

الحشر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢١

لَوْ أَنزَلْنَا هَـٰذَا ٱلْقُرْءَانَ عَلَىٰ جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُۥ خَـٰشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ ٱللَّهِ ۚ وَتِلْكَ ٱلْأَمْثَـٰلُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ ٢١

{21} Na pale Mwenyezi Mungu Mtukufu alipowabainishia waja wake yale aliyoyabainisha, na akawaamrisha na akawakataza waja wake katika Kitabu chake kitukufu, hili lilikuwa ni jambo la kuwafanya kuharakisha kufanya kile alichowaitia na akawahimiza juu yake, hata kama walikuwa wagumu na wenye mioyo migumu kama milima madhubuti. Kwani Qur-ani hii lau ingeteremshwa “juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu.” Hiyo ni kwa sababu ya athari yake kamili katika mioyo. Kwani mawaidha ya Qur-ani ndiyo mawaidha makubwa zaidi ya zama zote, na maamrisho yake na makatazo yake yana hukumu na masilahi yanayofungamana nayo, na ni miongoni mwa mambo mepesi zaidi kwa nafsi na miili, yasiyo na kujisumbua kukubwa, yasiyo na mgongano, wala kutofautiana, wala ugumu, wala kulazimishwa, ambayo yanafaa kwa kila wakati na mahali, na yanamfailia kila mtu. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akatuambia kuwa anawapigia watu mifano, na anawawekea wazi waja wake [katika Kitabu chake] halali na haramu; ili wazitafakari Aya zake na kuzizingatia. Kwani kuzitafakari kunamfungulia mja hazina za elimu, na kumbainishia njia za wema na uovu, na kunamhimiza juu ya maadili mema na mambo ya heshima, na kumkemea kutokana na maadili mabaya. Basi hakuna chenye manufaa zaidi kwa mja kuliko kuitafakari Qur-ani na kutafakari maana zake.