انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحشر
السورة ٥٩

الحشر

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٧

فَكَانَ عَـٰقِبَتَهُمَآ أَنَّهُمَا فِى ٱلنَّارِ خَـٰلِدَيْنِ فِيهَا ۚ وَذَٰلِكَ جَزَٰٓؤُا۟ ٱلظَّـٰلِمِينَ ١٧

{17} “Basi ikawa mwisho wa wote wawili hao.” Yaani, mwitaji, ambaye ni Shetani, na anayeitwa, ambaye ni mwanadamu, alipomtii “ni kuingia Motoni, wadumu humo daima.” Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Kwani yeye analiita kundi lake liwe katika watu wa Moto wenywe mwako mkali.’ Kisha akasema: “Na hayo ndiyo malipo ya madhalimu.” Wale walioshiriki katika dhuluma na ukafiri, hata wakitofautiana katika ukali na nguvu ya adhabu. Hii ndiyo desturi ya Shetani anavyowafanya marafiki wake wote. Kwani yeye huwaita na kuwabembeleza kwa hadaa hadi katika yale yatakayowadhuru, hata wanapotumbukia kwenye wavu wake na kuzingirwa na visababu vya maangamizo, anajitenga mbali nao na kuwaacha peke yao. Laki lawama zote zinawarudia wale wanaomtii. Kwani hakika Mwenyezi Mungu ameonya dhidi yake, na akajulisha kuhusu makusudio yake, malengo yake, na mwisho wake. Kwa hivyo mwenye kumtii, anakuwa ameasi baada ya kuwa na ufahamu na hana udhuru wowote.