المجادلة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ مِن قَبْلِ أَن يَتَمَآسَّا ۖ فَمَن لَّمْ يَسْتَطِعْ فَإِطْعَامُ سِتِّينَ مِسْكِينًا ۚ ذَٰلِكَ لِتُؤْمِنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ ۚ وَتِلْكَ حُدُودُ ٱللَّهِ ۗ وَلِلْكَـٰفِرِينَ عَذَابٌ أَلِيمٌ ٤
{4} “Na asiyepata mtumwa kumkomboa” au hakuweza kupata mali ya kumtolea utumwani, “basi” itamlazimu “afunge saumu miezi miwili mfululizo kabla hawajagusana. Na asiyeweza hayo” kufunga saumu, “basi awalishe masikini sitini.” Ima awalishe kutoka kwa chakula raisi cha nchini kwake kitakachowatosha; kama wanavyosema wafasiri wengi, na ima amlishe kila masikini viganja viwili vya ngano au chakula kinginecho kinachotosheleza katika Zakatul-fitr; kama ilivyo katika kauli ya baadhi ya madhehebu. “Hayo” ya hukumu tuliyokubainishieni ni “ili mumuamini Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Na hilo ni kwa kushikamana na hukumu hii na hukumu nyinginezo na kuzifanyia kazi. Kwani kushikamana na hukumu za Mwenyezi Mungu na kuzifanyia kazi ni katika imani. Bali ndilo hasa linalokusudiwa, na kwa hilo mja anazidisha imani yake na kuikuza na kuikamilisha. “Na hiyo ndiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu” ambayo inamzuia mtu kuanguka ndani ya makatazo yake, basi ni lazima isiivuke wala isipunguze chochote kwayo. “Na makafiri watapata adhabu chungu.”