المجادلة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يُظَـٰهِرُونَ مِنكُم مِّن نِّسَآئِهِم مَّا هُنَّ أُمَّهَـٰتِهِمْ ۖ إِنْ أُمَّهَـٰتُهُمْ إِلَّا ٱلَّـٰٓـِٔى وَلَدْنَهُمْ ۚ وَإِنَّهُمْ لَيَقُولُونَ مُنكَرًا مِّنَ ٱلْقَوْلِ وَزُورًا ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَعَفُوٌّ غَفُورٌ ٢
{2} "Wale miongoni mwenu wanaowasawazisha wake zao na mama zao, hao si mama zao. Hawakuwa mama zao ila wale waliowazaa." Na hili ni mwanamume kumwambia mkewe: 'Wewe mgongo wako ni kama mgongo wa mama yangu,' au wanawake wengineo ambao haruhusiwi kuwaoa, au aseme, 'Wewe ni haramu kwangu.' Lakini wao walikuwa wamezoea kutumia neno 'mgongo.' Basi akasema: "Wale miongoni mwenu wanaowasawazisha wake zao na mama zao, hao si mama zao." Yaani, vipi wanazungumza maneno haya ambayo wanajua kwamba hayana uhakika, kwa kuwafananisha wake zao na mama zao waliowazaa? Ndiyo maana Mwenyezi Mungu akachukulia hilo kuwa jambo kubwa mno, na akalifanya kuwa baya sana. Akasema: "Na hakika hao wanasema neno ovu mno, na la uwongo. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kughufiria mno, Mwenye kusamehe zaidi" kwa mwenye kufanya baadhi ya makosa kisha akayarekebisha kwa toba ya kweli.