الحديد
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱلَّذِينَ يَبْخَلُونَ وَيَأْمُرُونَ ٱلنَّاسَ بِٱلْبُخْلِ ۗ وَمَن يَتَوَلَّ فَإِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْغَنِىُّ ٱلْحَمِيدُ ٢٤
{24} "Ambao wanafanya ubahili, na wanaamrisha watu wafanye ubahili." Yaani, wanaunganisha vitu viwili vya kukashifiwa, kila kimoja kinatosha kuwa uovu mkubwa: ubakhili ambao ni kutotekeleza haki za faradhi, na tena wanawaamrisha watu kufanya hivyo. Kwa hivyo, ubakhili wao haukuwatosha wao mpaka wakawaamrisha watu pia kufanya hivyo, na kuwahimiza kufanya tabia hii ya kukadshifiwa, kwa maneno yao na vitendo vyao. Na hili ni katika kupeana kwao mgongo mambo ya kumtii Mola wao Mlezi na kugeuka kwao mbali nayo. "Na anayegeuka" akaacha kumtii Mwenyezi Mungu, basi hadhuru yeyote isipokuwa yeye mwenyewe, na wala hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu. "Kwani Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujitosha, Msifiwa mno." Yule ambaye kujitosheleza kwake ni katika sifa zisizoachana na dhati yake, ambaye miliki ya mbingu na ardhi ni yake, na ndiye aliyewatajirisha waja wake na kuwatosheleza. Naye ni msifiwa mno, Mwenye kila jina zuri, sifa kamili, tendo zuri analostahili kusifiwa juu yake na kutukuzwa.