انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحديد
السورة ٥٧

الحديد

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢١

سَابِقُوٓا۟ إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا كَعَرْضِ ٱلسَّمَآءِ وَٱلْأَرْضِ أُعِدَّتْ لِلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦ ۚ ذَٰلِكَ فَضْلُ ٱللَّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَآءُ ۚ وَٱللَّهُ ذُو ٱلْفَضْلِ ٱلْعَظِيمِ ٢١

{21} Kisha akatuamrisha tushindanie msamaha wa Mwenyezi Mungu, radhi yake, na bustani zake za mbinguni, na hiyo yanakuwa kwa kujitahidi kutafuta visababu vya msamaha, kama vile toba ya kweli, kuomba msamaha kwenye manufaa, kujiweka mbali na madhambi na sehemu zake, kushindana kufikia radhi za Mwenyezi Mungu kwa kufanya matendo mema, na kufanyia bidii daima yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu kama vile kumuabudu Muumba kwa uzuri, na kuwafanyia ihsani viumbe katika nyanja mbalimbali za manufaa, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu akataja matendo yanayosababisha hayo, akisema: "Na Bustani ya mbinguni ambayo upana wake ni kama upana wa mbingu na ardhi, iliyoandaliwa kwa ajili ya wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake." Kumuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake kunajumuisha misingi ya dini na matawi yake. "Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye." Yaani, haya tuliyokubainishieni na tukataja njia zinazofikisha katika bustani ya mbinguni na njia zinazofikisha katika Moto, na kwamba malipo ya Mwenyezi Mungu ambayo ni mengi na mazuri ni miongoni mwa neema zake kubwa kwa waja wake na fadhila zake. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye fadhila kuu." Ambaye sifa zake hazihesabiki zikadhibitiwa. Bali Yeye ni kama alivyojisifu mwenyewe, na yuko juu zaidi ya namna ambayo yeyote anamsifu miongoni mwa viumbe vyake.