انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحديد
السورة ٥٧

الحديد

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٩

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱللَّهِ وَرُسُلِهِۦٓ أُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلصِّدِّيقُونَ ۖ وَٱلشُّهَدَآءُ عِندَ رَبِّهِمْ لَهُمْ أَجْرُهُمْ وَنُورُهُمْ ۖ وَٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ وَكَذَّبُوا۟ بِـَٔايَـٰتِنَآ أُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلْجَحِيمِ ١٩

{19} "Na wale waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake" Imani kwa Masunni ni yale yaliyoashiriwa na Kitabu na Sunna, nayo ni maneno ya moyo na ulimi, na matendo ya moyo, ulimi na viungo. Na hayo yanajumuisha sheria zote za Dini zilizo dhahiri na zilizofichikana, kwa hivyo waliounganisha [baina ya] mambo haya "hao ndio Masidiqi (wakweli zaidi)" ambao daraja yao iko juu ya daraja za Waumini wote wa kawaida, lakini chini ya daraja za Manabii. Na kauli yake: "Na Mashahidi mbele ya Mola wao Mlezi. Wao watapata malipo yao na nuru yao." Kama ilivyokuja katika Hadithi sahihi: “Hakika kuna ngazi mia moja katika bustani za mbinguni, na umbali ulioko kati ya kila daraja mbili ni kama umbali uliopo kati ya mbingu na ardhi. Mwenyezi Mungu amewaandalia wanaofanya jihadi katika njia yake." Haya yanalazimu kwamba wako juu zaidi, na wametukuka zaidi na kwamba wako karibu zaidi na Mwenyezi Mungu. "Na wale waliokufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ndio wana Motoni." Aya hizi zimejumuisha aina za viumbe wanaotoa sadaka, wakweli zaidi, wale waliokufa katika njia ya Mwenyezi Mungu (mashahidi), na watu wa Motoni. Wale watoao sadaka, ni wale ambao walikuwa wakitoa na kuwapa viumbe na pia wakiwafanyia yenye kuwanufaisha kiasi wawezavyo, hasa kuwanufaisha kwa mali katika njia ya Mwenyezi Mungu. Nao wakweli ni wale waliokamilisha viwango vya imani, matendo mema, elimu yenye manufaa na yakini ya kweli. Nao mashahidi ni wale waliopigana katika njia ya Mwenyezi Mungu ili kuinua juu neno la Mwenyezi Mungu, wakajitolea nafsi zao na mali zao na wakauawa. Nao watu wa Motoni ni makafiri waliozikadhibisha Ishara za Mwenyezi Mungu. Na limebakia kundi lingine ambalo Mwenyezi Mungu alilitaja katika Surat Fatir, ambao ni wale wa katikati, ambao walitekeleza mambo ya wajibu na wakaacha yale yaliyoharamishwa. Hata hivyo, hawakufanya sawasawa baadhi ya haki za Mwenyezi Mungu na haki za waja wake. Hao pia marejeo yao yatakuwa katika bustani za mbinguni, hata kama baadhi yao wataadhibiwa kwa yale waliyoyafanya.