انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحديد
السورة ٥٧

الحديد

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٤

يُنَادُونَهُمْ أَلَمْ نَكُن مَّعَكُمْ ۖ قَالُوا۟ بَلَىٰ وَلَـٰكِنَّكُمْ فَتَنتُمْ أَنفُسَكُمْ وَتَرَبَّصْتُمْ وَٱرْتَبْتُمْ وَغَرَّتْكُمُ ٱلْأَمَانِىُّ حَتَّىٰ جَآءَ أَمْرُ ٱللَّهِ وَغَرَّكُم بِٱللَّهِ ٱلْغَرُورُ ١٤

{14} Kisha wanafiki watawaita Waumini, na waseme wakiomba kwa njia ya kusihi na kwa huruma kubwa: "Kwani hatukuwa pamoja nanyi" katika dunia, tukisema: Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, tukiswali, tukifunga, tukifanya jihadi, na kukifanya matendo kama yenu? "Watawaambia: Ndiyo," mlikuwa pamoja nasi katika dunia na mkatenda matendo kama sisi kwa dhahiri, lakini matendo yenu yalikuwa matendo ya wanafiki wasio na imani wala nia ya ukweli iliyo nzuri. "Lakini mlijifitini wenyewe, na mkatazamia mabaya (Waumini), na mkatia shaka" katika habari za Mwenyezi Mungu zisizo na shaka yoyote; "na matamanio ya nafsi zenu yakakudanganyeni." Ambapo mlikuwa mkitamani kupata yale watakayopata Waumini, na mkawa hata hamna yakini "mpaka ilipokuja amri ya Mwenyezi Mungu" ambayo ni mauti nanyi mko katika hali hiyo ya kukashifiwa; "na mdanganyifu yule akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu." Yaani, Shetani ndiye aliyekupambieni ukafiri na shaka, kwa hivyo mkatulia juu yake, na mkawa na imani na ahadi yake na mkasadiki habari zake.