انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الحديد
السورة ٥٧

الحديد

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١١

مَّن ذَا ٱلَّذِى يُقْرِضُ ٱللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَـٰعِفَهُۥ لَهُۥ وَلَهُۥٓ أَجْرٌ كَرِيمٌ ١١

{11} Kisha akawahimiza watu watoe na wapeane katika njia yake; Kwa sababu jihadi inategemea kutoa mali kwa ajili ya kuitayarisha. Basi akasema: "Ni nani atakayemkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema?" Ambao huwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu na wenye kuafikiana na radhi za Mwenyezi Mungu, kutokana na mali halali, nzuri na aliyotoa kwa moyo safi. Hili ni katika ukarimu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu; ambapo uliuita mkopo, ilhali mali hiyo ni yake, na waja pia ni waja wake, na akaahidi kuizidisha mali hiyo mizidisho mingi naye ndiye Mkarimu, Mpaji. Na mzidisho huo, mahali pake na siku yake ni siku ya Kiyama. Siku ambayo kila mtu atabainika uhitaji wake, na atahitaji malipo mazuri hata kidogo tu. Na ndiyo maana akasema: