الواقعة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلسَّـٰبِقُونَ ٱلسَّـٰبِقُونَ ١٠ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلْمُقَرَّبُونَ ١١ فِى جَنَّـٰتِ ٱلنَّعِيمِ ١٢ ثُلَّةٌ مِّنَ ٱلْأَوَّلِينَ ١٣ وَقَلِيلٌ مِّنَ ٱلْـَٔاخِرِينَ ١٤
{10 - 14} "Na wa mbele watakuwa mbele. Hao ndio watakaowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu)." Yaani, wa kwanza katika dunia kufanya wema ndio watakaokuwa wa kwanza Akhera kuingia katika bustani za mbinguni, wale wambao hizi ndizo sifa zao ndio watu wa karibu na Mwenyezi Mungu "katika Bustani zenye neema" katika walio juu kabisa, katika nyumba za juu kabisa ambazo hakuna daraja nyingine juu yake, na hao waliotajwa ndio "fungu kubwa katika wa mwanzo" kutoka katika umma huu na wengineo. "Na wachache katika wa mwisho." Na hili linaashiria ubora wa kizazi cha mwanzo cha umma huu kwa ujumla juu ya vizazi vyake vya baadaye. Kwa sababu walio karibu na Mwenyezi Mungu katika wale wa mwanzo ndio wengi zaidi kuliko wale wa baadaye, na walio karibu na Mwenyezi Mungu ndio viumbe maalumu.