انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الطور
السورة ٥٢

الطور

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٤٣

أَمْ لَهُمْ إِلَـٰهٌ غَيْرُ ٱللَّهِ ۚ سُبْحَـٰنَ ٱللَّهِ عَمَّا يُشْرِكُونَ ٤٣

{43} "Au wanaye mungu asiye kuwa Mwenyezi Mungu?" Yaani, je, wanaye mungu anayetarajiwa, ambaye yanatarajiwa manufaa yake na kuhofiwa madhara yake badala ya Mwenyezi Mungu? "Subhanallah (Ametakasika Mwenyezi Mungu) mbali na hao wanaowashirikisha naye." Yeye hana mshirika katika ufalme, wala hana mshirika katika umoja wake wala ibada zake. Na haya ndiyo yaliyokusudiwa katika maneno haya, nayo ni ubatili wa kuabudu kitu kingine chochote mbali na Mwenyezi Mungu, na kueleza uharibifu wake kwa hoja hizi za kukata kabisa, na kwamba hayo wayafanyayo washirikina ni batili, na kwamba yule anayepaswa kuabudiwa, kuswalia, kusujudia, na kutakasia dua ya ibada na dua ya kutaka kitu ni Mwenyezi Mungu, afanyiwaye uungu wa kweli, muabudiwa wa kweli, mkamilifu wa majina na sifa, mwingi wa sifa nzuri nyingi na matendo mazuri, mwenye heshima, ukarimu, na nguvu isiyoshindika, Mmoja, wa Pekee, Mkusudiwa, Mkubwa, Msifiwa mno, Mtukufu.