الطور
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَٱلْبَيْتِ ٱلْمَعْمُورِ ٤
{4} "Na kwa Nyumba iliyojengwa." Nayo ni Nyumba iliyo juu ya mbingu ya saba inayokaliwa daima na Malaika watukufu, ambayo huingiwa na Malaika elfu sabini kila siku, wakimuabudu humo Mola wa Mlezi, kisha hawarudi humo mpaka Siku ya Kiyama. Na imesemekana kwamba Al-Bayt Al-Ma'mur ni nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu (ya Makka), ambayo hujawa na wanaozunguka Tawafu, wanaoswali , na wanaomtaja Mola kila wakati, na wanaomjia kwa ajili ya Hija na Umra. Kama vile Mwenyezi Mungu alivyoapa kwayo katika kauli yake: "Na kwa mji huu wenye amani!" Basi inafilia zaidi kuapiwa na kubainishwa ukuu wake unaoifailia na utukufu wake nyumba iliyo bora kabisa miongoni mwa nyumba zilizo katika ardhi - ambayo wanaikusudia watu kwa ajili ya kufanya Hija na Umra, mojawapo ya nguzo za Uislamu na majengo yake makubwa, ambayo haukamiliki Uisilamu bila ya hiyo, na ndiyo iliyojengwa na Ibrahim na Ismail, na Mwenyezi Mungu akapafanya ni pahali pa kukusanyikia watu na pahala pa amani.