انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · الطور
السورة ٥٢

الطور

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢١

وَٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَٱتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَـٰنٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَآ أَلَتْنَـٰهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَىْءٍ ۚ كُلُّ ٱمْرِئٍۭ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ٢١

{21} Na hii ni miongoni mwa mambo yanayokamilisha neema za wana Peponi: kwamba Mwenyezi Mungu atawakutanisha na dhuria zao waliowafuata kwa Imani. Yaani, waliwafuata katika imani iliyotoka kwa baba zao. Kwa hivyo kizazi kikawa wafuasi wao katika imani, na muhimu zaidi ni ikiwa vizazi vyao vitawafuata kwa imani yao inayotokana na wa wenyewe. Watu hawa waliotajwa Mwenyezi Mungu atawakutanisha na vyeo vya baba zao Peponi, hata kama hawakuvifikia; yawe kama malipo kwa baba zao, na nyongeza ya ujira wao. Na pamoja na hayo Mwenyezi Mungu hatawapunguzia akina baba zao chochote katika matendo yao. Na kwa vile mtu anaweza kufikiri kuwa wana Motoni wao pia ni hivyo, kwamba Mwenyezi Mungu atawakutanisha na dhuriya zao, akajulisha kwamba hukumu ya nyumba mbili hizi si hukumu moja. Kwani Moto ni nyumba ya uadilifu. Na katika uadilifu wake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hamuadhibu yeyote isipokuwa kwa dhambi, na ndiyo maana akasema: "Kila mtu lazima atapata alichokichuma." Yaani, hakuna mbebaji hatambebea mwengine madhambi yake, na wala hakuna atakayebebeshwa mzigo wa mwingine. Hili limekusudiwa kuondoa dhana isiyokuwa ya kweli hiyo iliyotajwa.