ق
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا ۖ ذَٰلِكَ رَجْعٌۢ بَعِيدٌ ٣ قَدْ عَلِمْنَا مَا تَنقُصُ ٱلْأَرْضُ مِنْهُمْ ۖ وَعِندَنَا كِتَـٰبٌ حَفِيظٌۢ ٤
{3 - 4} Kisha akataja sababu ya mshangao wao, akasema: "Ati tukifa na tukawa udongo...? Kurejea huko kuko mbali!" Hapo walilinganisha uwezo wa Mwenye uwezo zaidi juu ya kila kitu, Mkamilifu kwa namna zote kwa uwezo wa mja mhitaji asiyejiweza kwa namna zote! Wakamlinganisha mjinga asiye na elimu na Yule anayejua zaidi kila kitu, ambaye anajua "kiasi cha kila kinachopunguzwa na ardhi," kama vile miili yao muda wa kukaa kwao kaburini, na amedhibiti katika kitabu chake ambacho kiko kwake - kilichohifadhiwa kutokana na mabadiliko na mageuzi - kila kitu kitakachowatokea katika maisha yao na baada ya kifo chao. Huku ni kutumia ushahidi wa ukamilifu wa upana wa elimu yake, ambao hakuna anayeweza kuudhibiti isipokuwa Yeye, juu ya uwezo wake wa kuwafufua wafu.