المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
ٱعْلَمُوٓا۟ أَنَّ ٱللَّهَ شَدِيدُ ٱلْعِقَابِ وَأَنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ٩٨
{98} "Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkali wa kuadhibu, na ya kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Yaani, na ziwe elimu mbili hizi zinapatikana katika nyoyo zenu kwa namna ya uhakika na yakini. Mjue ya kwamba Yeye ni Mkali wa kuadhibu, sasa na baadaye kwa mwenye kumuasi, na kwamba Yeye ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kumrehemu mwenye kutubia kwake na akamtii. Basi elimu hii ikawaletea hofu ya adhabu yake, na kutumaini kufuta kwa dhambi na thawabu zake. Na mtende kulingana na yale yanayotakiwa na hofu hiyo na matumaini.