انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٨٧

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تُحَرِّمُوا۟ طَيِّبَـٰتِ مَآ أَحَلَّ ٱللَّهُ لَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ ٱلْمُعْتَدِينَ ٨٧

{87} Anasema Yeye Mtukufu; "Enyi mlioamini! Msiviharimishe vizuri alivyowahalalishia Mwenyezi Mungu" miongoni mwa vyakula na vinywaji. Kwa sababu hivyo ni neema alizowaneemesha kwazo Mwenyezi Mungu. Basi msifuni anapowahalalishia hizo na mshukuruni, wala msiirudishe neema yake kwa kuikufuru, au kwa kutoikubali, au kwa kuitakidi kuwa ni haramu. Kwa hivyo mkawa mmechanganya kwa hilo kati ya kusema uongo juu ya Mwenyezi Mungu na kukufuru neema yake, na kuitakidi kile kilicho halali na kizuri kuwa ni haramu na kiovu. Kwa maana hili ni katika kuvuka mipaka. Na Mwenyezi Mungu amekataza kuvuka mipaka, kwa hivyo akasema; "wala msipite mipaka. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wavukao mipaka." Bali anawachukia na anawachukia na anawaadhibu kwa hilo.