المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
كَانُوا۟ لَا يَتَنَاهَوْنَ عَن مُّنكَرٍ فَعَلُوهُ ۚ لَبِئْسَ مَا كَانُوا۟ يَفْعَلُونَ ٧٩
{79} Na miongoni mwa maasia yao yaliyowaletea adhabu ya kupigiwa mfano, ikafikishia mateso ni kwamba “Walikuwa hawakatazani maovu waliyokuwa wakiyafanya.” Yaani walikuwa wakifanya maovu na hawakatazani wenyewe kwa wenyewe, kwa hivyo wanashiriki katika hilo wale walioyafanya hasa, na wengineo ambao walinyamazia kukataza maovu pamoja na kuwa kwao na uwezo juu ya hilo. Na hilo hilo linaashiria kuzembea kwao na amri ya Mwenyezi Mungu, na kwamba kumuasi ni kitu rahisi kwao. Kwa maana, lau kuwa wangekuwa wanamtukuza Mola wao Mlezi, basi wangeona ghera kwa sababu ya kufanywa kwa maharamisho yake, na wangekasirika kwa sababu ya kukasirika kwake. Na kulikuwa kukaa kimya juu ya uovu pamoja na kuwa na uwezo wa kukataza ni kwenye kusababisha adhabu, kwa sababu ya uharibifu mkubwa ambao uko ndani yake: Na miongoni mwake ni kwamba kunyamaza kimya ni kutenda maasia, hata kama mtu huyo aliye kimya hakuyafanya hasa. Kwa maana, kama vile inavyopasa kujiepusha na maasia; basi inapasa kukataza mwenye kufanya maasia. Na miongoni mwake ni yale yaliyotangulia kuwa inaashiria kuyafanyia uzembe maasia, na uchache wa kuyajali. Na miongoni mwake ni kwamba hilo linawahimiza waasi na wenye kupita mipaka kufanya maasia ikiwa hawatazuiliwa kuyafanya. Kwa hivyo uovu unaongezeka, na balaa ya kidini na ya kidunia inakuwa kubwa zaidi, na wanapata nguvu na ushindi. Kisha baada ya hayo watu wema wanakufa dhaifu katika kuwapinga watu waovu, mpaka wasiweze kufanya yale waliyokuwa wanaweza kufanya hapo mwanzo. Na miongoni mwake ni kwamba, Katika kuacha kukataza maovu elimu inadidimia, na ujinga unaongezeka. Kwa maana maasia pamoja na kurudiarudia kwake, na kufanywa kwake na watu wengi, na watu wa dini na elimu kutoyakataza, inadhaniwa kuwa si maasia, na huenda mjinga akadhani kuwa ni ibada inayopendekezwa. Na ni uharibifu gani ulio mkubwa zaidi kuliko kuitakidi kuwa, alichoharamisha Mwenyezi Mungu ni halali, na kugeuka kwa uhakika katika nafsi, na kuiona batili kwamba ni haki? Na miongoni mwake ni kwamba kukaa kimya juu ya maasia ya waasi kunaweza maasia yakajipamba katika nyoyo za watu, na wakaigana wao kwa wao. Kwa maana, mwanadamu hupenda kuiga wale walio mfano wake na watu wa jinsi yake... na miongoni mwake, na miongoni mwake... Na pindi kunyamazia kukataza kupolikuwa katika nafasi hii, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema moja kwa moja kuwa aliwalaani makafiri miongoni mwa Wana wa Israili kwa maasia yao na kupita kwao mipaka. Na akataja kwa namna mahususi uovu huu mkubwa: "Ni maovu mno waliyokuwa wakiyafanya."