المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
قُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لَا تَغْلُوا۟ فِى دِينِكُمْ غَيْرَ ٱلْحَقِّ وَلَا تَتَّبِعُوٓا۟ أَهْوَآءَ قَوْمٍ قَدْ ضَلُّوا۟ مِن قَبْلُ وَأَضَلُّوا۟ كَثِيرًا وَضَلُّوا۟ عَن سَوَآءِ ٱلسَّبِيلِ ٧٧
{77} Mwenyezi Mungu Mtukufu anamwambia Nabii wake - rehema na amani zimshukie - "Sema enyi Watu wa Kitabu, msipitie kiasi katika dini yenu bila ya haki." Yaani, msipite mipaka, na kukiuka haki kwenda kwenye batili. Na hilo ni kama kauli yao kuhusiana na Masihi kama ilivyotangulia kusimulia juu yao, na kama kuzidi kwao kiasi katika baadhi ya mashekhe kwa kufuata matamanio ya "kaumu waliokwisha potea tangu zamani." Yaani, upotovu wao ulikwisha tangulia, "na wakawapoteza wengi" miongoni mwa watu kwa kuwalingania kwenda katika dini ambayo wako juu yake; "Na wenyewe wakapotea njia iliyo sawa;" yaani, alikusudia njia. Kwa hivyo, wakachanganya kati ya upotovu na kupotosha na hawa ndio maimamu wa upotovu ambao Mwenyezi Mungu alionya dhidi yao, na dhidi ya kufuata matamanio yao yenye kuangamiza na rai zao zenye kupotosha.