المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
أَفَلَا يَتُوبُونَ إِلَى ٱللَّهِ وَيَسْتَغْفِرُونَهُۥ ۚ وَٱللَّهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ٧٤
{74} Kisha akawaita watubu kwa yale waliyoyatenda, na akabainisha kuwa Yeye hakika anakubali toba kutoka kwa waja wake. Kwa hivyo akasema; "Basi je, hawatatubii kwa Mwenyezi Mungu." Yaani warejee katika yale anayoyapenda na kuyaridhia, kama vile kumkiria Mwenyezi Mungu upweke, na kwamba Isa ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kuacha yale waliyokuwa wakiyasema; "na wakamwomba awafutie dhambi" kwa yale waliyoyatenda. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kufuta dhambi, Mwenye kurehemu." Yaani Anafuta madhambi ya waliotubu hata kama yatafikia upande wa juu wa mbingu. Na Anawarehemu kwa kuwakubalia toba yao, na kuyabadilisha mabaya yao kuwa mema. Na alianza katika kuwaita kutubia kwa mbinu ambayo ni ya hali ya juu zaidi ya upole na ulaini katika kauli yake; “Basi je, hawatatubii kwa Mwenyezi Mungu?"