المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَحَسِبُوٓا۟ أَلَّا تَكُونَ فِتْنَةٌ فَعَمُوا۟ وَصَمُّوا۟ ثُمَّ تَابَ ٱللَّهُ عَلَيْهِمْ ثُمَّ عَمُوا۟ وَصَمُّوا۟ كَثِيرٌ مِّنْهُمْ ۚ وَٱللَّهُ بَصِيرٌۢ بِمَا يَعْمَلُونَ ٧١
{71} "Na wakadhani kuwa hapatakuwa majaribio." Yaani, walidhani kuwa uasi wao na kukadhibisha kwao hakutawaletea adhabu wala mateso, na wakaendelea na batili yao, na wakawa vipofu "na viziwi" kuielekea haki. "Kisha" akawainua na "akawapokelea toba zao" walipotubia kwake na wakarudi kwake. "Kisha" hawakuendelea hivyo mpaka wengi wao wakaigeukia ile hali mbaya. Basi, "tena wengi katika wao wakawa vipofu na viziwi" kwa maelezo haya, na wachache wakaendelea katika toba na imani yao. "Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona vyema hayo wayatendayo;" na atamlipa kila mtendaji kwa matendo yake, ikiwa ni heri, basi kwa heri, na ikiwa ni uovu, basi kwa uovu.