انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٦٨

قُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ لَسْتُمْ عَلَىٰ شَىْءٍ حَتَّىٰ تُقِيمُوا۟ ٱلتَّوْرَىٰةَ وَٱلْإِنجِيلَ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ ۗ وَلَيَزِيدَنَّ كَثِيرًا مِّنْهُم مَّآ أُنزِلَ إِلَيْكَ مِن رَّبِّكَ طُغْيَـٰنًا وَكُفْرًا ۖ فَلَا تَأْسَ عَلَى ٱلْقَوْمِ ٱلْكَـٰفِرِينَ ٦٨

{68} Yaani, Waambie Watu wa Kitabu ukiuita upotovu wao na ukitangaza batili yao, "Hamko katika chochote" katika mambo ya kidini. Kwani nyinyi hamkuamini si Qur-ani wala Muhammad, wala hamukusadiki si Nabii wenu wala kitabu chenu, wala hamukushikamana na haki yoyote, wala hamkutegemea juu ya msingi wowote. "Mpaka muisimamishe Taurati na Injili." Yaani, mvifanye visimame kwa kuviamini, na kuvifuata, na kushikamana na kila vinachokilingania. "Na" myasimamishe "yote mliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wenu Mlezi" ambaye aliwalea, na akawaneemesha, na akaifanya tukufu zaidi ya neema yake juu yenu ni kuwateremshia Vitabu. Basi la wajibu juu yenu ni kwamba mumshukuru Mwenyezi Mungu, na mshikamane na hukumu za Mwenyezi Mungu, na mtekeleze yale mliyokabidhiwa miongoni mwa amana ya Mwenyezi Mungu na ahadi yake. "Na hakika uliyoteremshiwa wewe kutoka kwa Mola wako Mlezi yatawazidishia wengi katika wao uasi na ukafiri. Basi usiwasikitikie kaumu ya makafiri."