انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٩

قُلْ يَـٰٓأَهْلَ ٱلْكِتَـٰبِ هَلْ تَنقِمُونَ مِنَّآ إِلَّآ أَنْ ءَامَنَّا بِٱللَّهِ وَمَآ أُنزِلَ إِلَيْنَا وَمَآ أُنزِلَ مِن قَبْلُ وَأَنَّ أَكْثَرَكُمْ فَـٰسِقُونَ ٥٩

{59} Yaani, "Sema" ewe Mtume: "Enyi Watu wa Kitabu"! Ukiwalazimishia hakika Dini ya Uislamu ndio Dini ya haki, na mkiikashifu, basi huko ni kukashifu jambo linalostahiki kusifiwa. "Je, mnatuchukia isipokuwa tu kwamba tulimwamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyoteremshiwa na yale yaliyoteremshwa kabla, na kwa kuwa wengi wenu ni wapitao mipaka?" Yaani, Je, tuna kasoro yoyote isipokuwa kumwamini kwetu Mwenyezi Mungu, na katika vitabu vyake vilivyotangulia na vilivyofuatia, na Manabii wake wa mwanzo na wa mwisho? Na kwamba tuna hakika kwamba asiyeamini imani hii, basi yeye ni kafiri na aliyepita mipaka. Basi je, mnatuchukia kwa hili, ambalo ndilo wajibu wa wajibu zote juu ya kila anayewajibika kisheria? Hata hivyo, wengi wenu ni " wapitao mipaka." Yaani, watokao katika utii wa Mwenyezi Mungu, wanaofanya ujasiri wa kumuasi. Basi ni bora zaidi kwenu, enyi wapitao mipaka kunyamaza. Na lau kuwa kutukashifu kwenu kulifanyika hali ya kuwa mko salama kutokana na kupita mipaka, na ni mbali sana hilo, basi uovu ungekuwa mwepesi zaidi kuliko kutukashifu kwenu pamoja na kupita kwenu mipaka.