انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥١

يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ لَا تَتَّخِذُوا۟ ٱلْيَهُودَ وَٱلنَّصَـٰرَىٰٓ أَوْلِيَآءَ ۘ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَآءُ بَعْضٍ ۚ وَمَن يَتَوَلَّهُم مِّنكُمْ فَإِنَّهُۥ مِنْهُمْ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلظَّـٰلِمِينَ ٥١

{51} Yeye Mtukufu anawaelekeza waja wake Waumini wakati anapowabainishia hali za Mayahudi na Wakristo na sifa zao zisizokuwa nzuri kwamba wasiwafanye kuwa marafiki wandani. Kwa sababu wao kwa wao "ni marafiki wandani," wanaonusuriana wao kwa wao, na wao ni mkono mmoja juu ya asiyekuwa wao. Basi nyinyi msiwafanye kuwa marafiki wandani. Kwa sababu ni maadui kwa hakika, na wala hawajali kuwadhuru, bali hawaweki kando katika juhudi zao chochote katika kuwapotosha nyinyi. Wala hawawafanyi kuwa marafiki wandani isipokuwa yule ambaye ni kama wao. Na ndiyo maana akasema, "Na mwenye kuwafanya marafiki wandani miongoni mwenu, basi huyo hakika ni miongoni mwao." Kwa sababu kuwafanya kuwa marafiki wandani kukamilifu kunalazimu kubadilika na kwenda katika dini yao. Na kuwafanya kuwa wandani kidogo tu kunaitia mengi, kisha kunaongezeka polepole, mpaka mja anakuwa miongoni mwao. "Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu wenye kudhulumu," yaani, wale ambao sifa yao ni dhuluma, na kwayo wanarejeshwa, na kwayo wanategemea. Na lau utawaletea kila Aya, hawawezi kukufuata, wala kukutii.