المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَقَفَّيْنَا عَلَىٰٓ ءَاثَـٰرِهِم بِعِيسَى ٱبْنِ مَرْيَمَ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ ۖ وَءَاتَيْنَـٰهُ ٱلْإِنجِيلَ فِيهِ هُدًى وَنُورٌ وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ مِنَ ٱلتَّوْرَىٰةِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةً لِّلْمُتَّقِينَ ٤٦
{46} Yaani, na tuliwafuatisha Manabii hawa na Mitume hawa ambao wanahukumu kwa Taurati kwa mja wetu na Mtume wetu Isa bin Maryam, roho wa Mwenyezi Mungu na neno lake alilozungumza kwalo kwa Maryam. Mwenyezi Mungu akamtuma kusadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Taurati. Basi Yeye ni shahidi wa Musa na yale aliyoyaleta katika Taurati kwamba ni ya haki na ukweli, na yenye kuunga mkono kulingania kwake, na mwenye kuhukumu kwa sheria yake, na mwenye kuafikiana naye katika mengi ya mambo ya kisheria. Na Isa, amani iwe juu yake, huenda aliepesisha katika baadhi ya hukumu. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu alivyosema kumhusu kwamba aliwaambia Wana wa Israili, "na ili niwahalalishie baadhi ya yale mliyoharimishiwa," "na tukampa Injili;" Kitabu kitukufu kinachoikamilisha Taurati. "Iliyomo ndani yake uwongofu, na ni nuru" inayoongoza kwenye njia iliyonyooka, na inabainisha haki kutokana na batili. "Na inayosadikisha yale yaliyokuwa kabla yake katika Taurati," kwa kuithibitisha, na kuishuhudia, na kuafikiana nayo. "Na ni uwongofu na mawaidha kwa wachamungu," kwani hao ndio wenye kunufaika na uwongofu, na wanawaidhika kwa mawaidha, na wakajiepusha na yasiyofaa.