المائدة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
فَطَوَّعَتْ لَهُۥ نَفْسُهُۥ قَتْلَ أَخِيهِ فَقَتَلَهُۥ فَأَصْبَحَ مِنَ ٱلْخَـٰسِرِينَ ٣٠
{30} Lakini huyo mkosaji hakuzuilika, wala hakukomeka, na hakuacha kuiazimia nafsi yake na kufanya uamuzi imara, mpaka ikampelekea kumuua kaka yake ambaye sheria na maumbile vinahitaji aheshimiwe. "Na akamuua. Kwa hivyo akawa miongoni mwa waliohasiri" dunia yao na Akhera yao. Na akawa ameweka nyendo hii kwa kila muuaji. Na mwenye kuweka nyendo mbaya, basi mzigo wake uko juu yake na mzigo wa mwenye kufanya hivyo mpaka Siku ya Qiyama. Na ndiyo maana ilikuja katika hadithi Sahihi kuwa: “Hakuna nafsi yoyote itakayouawa, isipokuwa inakuwa juu ya mwana wa kwanza wa Adamu nusu ya damu yake; Kwa sababu yeye ndiye aliyeweka nyendo ya kuua.”