انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٢٤

قَالُوا۟ يَـٰمُوسَىٰٓ إِنَّا لَن نَّدْخُلَهَآ أَبَدًا مَّا دَامُوا۟ فِيهَا ۖ فَٱذْهَبْ أَنتَ وَرَبُّكَ فَقَـٰتِلَآ إِنَّا هَـٰهُنَا قَـٰعِدُونَ ٢٤

{24} Lakini maneno haya hayakuwaathiri, wala haikuwafaa lawama, na wakasema maneno ya wanyonge. "Ewe Musa! Hakika Sisi hatutaingia humo kamwe maadamu wao wamo humo. Basi nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane. Sisi hakika tutakaa papa hapa." Basi ni kauli iliyo mbaya zaidi gani hii kutoka kwao, na kukabiliana kwao na Nabii wao mahali hapa pagumu, pafinyu, ambapo haja na dharura inataka wamuunge mkono Nabii wao na kujitukuza nafsi zao? Basi kwa hili na mfano wake inadhihirika tofauti kati ya umma zote na umma wa Muhammad – rehema na amani ziwe juu yake – ambapo maswahaba walimwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu - rehema na amani ziwe juu yake; – alipotaka ushauri wao kuhusu kupigana katika vita vya Siku ya Badr, ingawa hakuwaamulia amri ya mkazo juu hilo: 'Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Lau kuwa utaingia nasi katika bahari hii; basi tungeingia humo pamoja nawe. Na lau kuwa ungefika Barak Al-Ghamad pamoja nasi, basi hangebaki nyuma yeyote, wala hatusemi kama walivyomwambia Musa watu wa Musa: Nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane, sisi tumekaa papa hapa. Lakini nenda wewe na Mola wako Mlezi mkapigane, hakika sisi tuko pamoja nanyi tunapigania mbele yako na nyuma yako, na kulia kwako na kushoto kwako.