انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · المائدة
السورة ٥

المائدة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ١٨

وَقَالَتِ ٱلْيَهُودُ وَٱلنَّصَـٰرَىٰ نَحْنُ أَبْنَـٰٓؤُا۟ ٱللَّهِ وَأَحِبَّـٰٓؤُهُۥ ۚ قُلْ فَلِمَ يُعَذِّبُكُم بِذُنُوبِكُم ۖ بَلْ أَنتُم بَشَرٌ مِّمَّنْ خَلَقَ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَآءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَآءُ ۚ وَلِلَّهِ مُلْكُ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ وَإِلَيْهِ ٱلْمَصِيرُ ١٨

{18} Na Miongoni mwa maneno ya Mayahudi na Manasara ni kwamba kila mmoja wao alidai madai ya batili ambayo kwayo wanazitakasa nafsi zao kwayo. Kwamba kila mmoja wao alisema: "Sisi ni wana wa Mwenyezi Mungu na vipenzi vyake." Na Ibn katika lugha yao ni mpenzi, na hawamaanishi uwana wa kihakika. Kwani hili si katika dhehebu lao isipokuwa dhehebu la Kikristo kuhusiana na Masihi. Mwenyezi Mungu akawajibu kwa sababu walidai bila ya ushahidi, "Sema, basi kwa nini anawaadhibu kwa sababu ya dhambi zenu?" Ikiwa mngekuwa vipenzi vyake, hangewaadhibu, kwa sababu Mwenyezi Mungu hawapendi isipokuwa wale wanaofanya yale anayoridhia. "Bali nyinyi ni wanadamu tu kama wale wengine aliowaumba." Zinawapitikia hukumu za uadilifu na fadhila, "Humfutia dhambi amtakaye na humuadhibu amtakaye;" ikiwa watafanya sababu za kufutiwa dhambi au adhabu. "Na ni wa Mwenyezi Mungu tu ufalme wa mbingu na ardhi. Na marejeo ni kwake Yeye." Yaani, ni nini kilichofanya fadhila hizi kuwa mahususi kwenu tu na hali nyinyi ni miongoni mwa wale anaowaamili na miongoni mwa wale watakaorudi kwa Mwenyezi Mungu katika Nyumba ya Akhera, na awalipe kwa matendo yenu?